Shirika la kimataifa la kawi ya kitonoradi, limedhibitisha kuwa shughuli za kurutubisha madini hayo zinaendelea katika kiwanda hicho cha Fordo.Wakuu wa serikali ya marekani mjini Washington wanasema tangazo hilo la Iran ni uchochezi.Victoria Nuland, msemaji katika ofisi ya rais anasema kiwango hicho kikubwa cha kurutubisha madini ya uranium kimechochea zaidi hofu zao kuhusu madai kuwa mradi huo wa Iran wa nyuklia ni wa amani.Anasema madini ya Uranium yakirutubishwa hadi kiwango cha asilimia 20, huwa sawa na silaha.Naye waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hague, amesema kuhusu hatua hizi za Iran wakati ambapo jumuiya ya kimataifa imekuwa ikiisihi Tehran itoe maelezo kuhusu mradi huo ni za uchokozi.Kwa muda wa miezi kadhaa sasa uhusiano kati ya Iran na nchi za magharibi umekuwa mbaya. Wiki iliopita marekani iliiwekea vikwazo benki kuu ya nchi hiyo na Umoja wa Ulaya ulitangaza kuzuia mauzo ya mafuta ya Iran.Kufuatia hatua hizo, nayo Iran ilitishia kufunga mkondo wa bahari wa Hormuz ambapo zaidi ya asilimia 20 ya mafuta kote duniani hupitia.
19 Machi 2011 - 20:30
Msimbo wa Habari: 289987
ABNA inatuarifu kuwa: Taarifa ya Iran kuanza kurutubisha Uraniam imekuwa gumzo duniani hasa kwa Marekani. Iran imeanza kurutubisha madini ya Uranium katika kiwanda kilichoko chini ya ardhi kaskazini mwa nchi hiyo.